Loading...

Jul 4, 2020

Trump: Kuondolewa kwa sanamu za viongozi mbalimbali kulilenga kufuta historia


Rais Donald Trump amezungumza kuhusu vitendo vya kuondolewa kwa sanamu za viongozi mbalimbali nchini humo akisema ni kampeni iliyolenga kufuta historia

Ameongeza kuwa vitendo hivyo vilivyofanywa na umati wa watu wenye hasira wakati wa maandamano vililenga kuwashusha hadi mashujaa wa taifa hilo, na waliohusika wanaweza kuhukumiwa kifungo cha hadi miaka 10

Amesema hayo akiwa Mlima Rushmore kwa ajili ya maadhimisho ya Uhuru ya Julai 04, hafla ambayo imehudhuriwa na watu takriban 7,500 huku kukiwa hakuna tahadhari zozote za kujikinga na COVID19

Licha ya rekodi mpya ya maambukizi, Rais Trump alizungumzia mlipuko huo mwa ufupi. Hafla haikuzingatia umbali salama na wahudhuriaji hawakulazimika kuvaa barakoa

Wakati huo huo, imeripotiwa kuwa Afisa wa juu wa kampeni ya Trump, Kimberly Guilfoyle ambaye pia ni Mpenzi wa mtoto wa Rais huyo, Donald Trump Jr. ameambukizwa Corona
KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger