Umoja wa Ulaya utadhibiti bidhaa za teknolojia ambayo inaweza kutumika kwa ukandamizaji au uchunguzi wa umma huko Hong Kong. Kwa mujibu wa rasimu ya umoja huo ambayo nakala yake imeweza kuonwa na Reuters, mapendekezo yake yanaweza kuanza kutelezwa Jumanne ijayo.
Wakieleza masikitiko yao kutokana na uwepo wa sheria ya usalama wa taifa ya China, kwa koloni la zamani la Uingereza Hong Kong, mataifa 27 ya Umoja wa Ulaya yamekubalina kuweka vikwazo kadhaa vikiwemo udhibiti wa kibiashara na kufanya mapitio ya sheria ya hati za kusafiria kwa mamlaka hiyo.
Hong Kong ilikuwa na dhamana ya uhuru wa mpana wakati ikirejeswa kwa utawala wa China mnamo 1997.
