Na Ahmad Mmow, Lindi.
Rais mstahafu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wa awamu ya nne, Dkt Jakaya Kikwete ametoa wito kwa wananchi waendeleze mshikamano, undugu, amani na utulivu uliopo nchini hata baada ya kumalizika uchaguzi mkuu wa mwaka huu wa 2020.
Dkt Kikwete ametoa wito huo jana mjini Lindi alipowasalimia waumini wa dini ya kiislam katika uwanja wa mpira wa miguu wa Ilulu mara baada yakumalizika swala ya Iddi.
Dkt Kikwete alisema kipindi cha kujiandikisha kwa ajili ya uchaguzi huo kimepita. Lakini licha ya kutunza shahada zao za kupigia kura, pia wadumishe undugu, mshikamano, amani na utulivu uliopo nchini hata baada ya uchaguzi huo kumalizika.
Dkt Kikwete alionya kuwa uchaguzi huo usiwe nongwa na kusababisha kuharibu amani na utulivu.
'' Uchaguzi usiwe kichocheo cha kuvuruga amani na utulivu. Uchaguzi uwe wa amani bila kutukanana na kuhasimiana ili baada ya kwisha tuendelee kuwa ndugu, uchaguzi usiwe nongwa,'' alisisitiza Dkt Kikwete.
Mbali na hayo, Rais mstahafu huyo wa awamu ya nne alitoa wito kwa wananchi wa mikoa ya Lindi na Mtwara wajipange kupokea fursa zitakazotokana na ujenzi wa mtambo wa kuchakata gesi asilia unatorajiwa kujengwa katika mtaa wa Likong'o, manispaa ya Lindi.
Alisema mkoa wa Lindi ni miongoni mwa mikoa isiyopiga hatua kubwa ya maendeleo. Kwahiyo ujenzi wa mtambo huo katika eneo hilo uwe kichocheo cha maendeleo ya mikoa hiyo.
Alionya kwamba wasipojipanga wanaweza kushindwa kufaidi na kunufaika na fursa zitakazo tokanana ujenzi wa mtambo huo. Badala yake watakuwa walalamikaji na wanung'unikaji wakati ambao watu watakaojipanga vizuri watakapofaidika.
'' Naamini viongozi watakaa chini na kutafakari jinsi gani wananchi watanufaikana kichocheo hicho cha maendeleo,'' alisisitiza Dkt Kikwete.
Mstahafu huyo alitaja eneo moja kati ya mengi yanayoweza kuwa ni miongoni mwakujipanga ni wekeza kwenye sekta ya elimu.
Kuhusu hilo, alibainisha kwamba mkoa wa Lindi ni miongoni mwamikoa iliyo nyuma kielimu. Hivyo nirahisi watoto wa mkoa huo kuwa watazamaji badala ya kushiriki na kufaidi matunda ya gesi asilia iliyogunduliwa katika kanda hiyo ya Kusini.