Shujaa' wa filamu ya Hoteli Rwanda atapewa haki kisheria, yasema Rwanda


Msemaji wa uendeshaji mashitaka wa umma nchini Rwanda ameihakikishia familia kuwa ‘‘shujaa’’ wa filamu ya Hoteli Rwanda na mpinzani wa nchini hiyo Paul Rusesabagina atapata haki ya kisheria katika kesi dhidi yake inayoendelea.

‘’Hata alipokamatwa ilitangazwa wazi...alipouguwa alipata huduma ya matibabu, alipewa jopo la mawakili tena bure… Kesi itakuwa wazi kwa umma.’’ Amesemamsemaji wa ofisi yauendeshaji mashitaka ya umma nchini Rwanda Paul Nkusi katika mahojiano na kipindi cha BBC Newsday

Bwana Nkusi amesema, la muhimu ni kwamba alikamatwa katika uwanja wa ndege wa Rwanda na sasa yuko mikononi mwa polisi ili aweze kujibu mashitaka yanayomkabili.

Bwana Rusesabagina anakabiliwa na mashitaka ya mauaji ya raia, kuwajeruhi raia, kupora na kuharibu mali za raia, kuunda kundi lenye silaha hususan ni FNL ambalo linawatumikisha watoto vitani, na kuhusika katika shuguli za ugaidi, amesema Bwana Nkusi.

Nkusi amesema Rusesabagina binafsi alithibitisha mwenyewe kuhusika katika baadhi ya vitendo hivi.

‘’Ninaweza kutaja baadhi ya ushahidi aliousema mwenyewe…alisema alituma pesa kwa njia ya Western Union na kukusanya pesa za kuunga mkono kikundi cha FNL’’, Alisema Bwana Nkusi.

Familia ya Rusesababigina ambaye alipata umaarufu baada ya kucheza filamu ya Hoteli Rwanda juu ya mauaji ya kimbari ya Rwanda, inasema kuwa alitekwa nyara alipokuwa safarini Dubai katika Muungano wa nchi za kiarabu.

Msemaji huyo wa Ofisi ya mwendesha mashitaka ya umma amesema kuwa kwasasa anashikiliwa katika kituo cha polisi Remera na mawakili wake wanamtembelea.

Post a Comment

0 Comments