Asasi za kiraia Mkoani Mtwara watoa tamko la kulaani vitendo vya ukandamizaji ,uonevu na udhalilishaji kwa wanawake


Na Faruku Ngonyani ,Mtwara           

Shirika la Door Of Hope Tanzania kwa Kushirikiana na Asasi za Kiraia Mkoani Mtwara wametoa tamko la kulaani vitendo vya ukandamizaji ,Uonevu na udhalilishaji wa wananwake unaofanywa na baadhi ya wagombea wanpokuwa jukwaani.

MKugurenzi wa Shirika la Door of Hope Tanzania Tanzania Clemence Mwombeki amesema kuwa uchaguzi wa mwaka huu kumekuwa na idadi kubwa ya wananwake wanaowania nafasi mbali mbali za uongozi ukilinganisha na uchaguzi uliopita.

Aidha ameongeza kuwa kwa kampeni zinazoendelea hapa nchini kwa uchaguzi Mkuu ,kumekuwa na vitendo vya ukandamizaji ,usumbufu usiokuwa wa lazima ,Mizengwe pamoja unyanyasasi wa kijinsia kwa wananwake.

“Tumeona na kusikia sana vitendo vya ukandamizaji ,usumbufu usiokuwa wa lazima ,mizengengo na mambo mengine yanayofanywa na baadhi ya wagombea wa napokuwa jukwaani”

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Faidika wote pamoja (FAWOPA) Baltazal Komba ameeleza kuwa  baadhi ya wagombea kwenye majukwaa wamekuwa wakitamka maneno ya kuwadhalilisha wananwake lakini pia wanawachulia wanawake sehemu ya kuwatolea mifano mba mbali.

Aidha Komba ametoa wito kwa viongozi wa vyama vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi Mkuu hapa nchini kuwakemea wagombea wao lakini kuwaomba msamaha wanawake kutokana na kazi kubwa wanayoifanya.

“Tumeona baadhi ya wagombea kwenye majukwaa wakitamka maneno ya kuwadhalilisha wanawake ,Tumeona baadhi ya wagombea kwenye majukwaa wakiwachukulia wanawake kama sehemu ya kuwatolea mifano,sisi kwetu kama mashirika yasio ya kiserikali tumeona hiyo sio sawa”

Aidha Komba amechukua fursa hiyo kwa kuwapongeza jeshi la polisi kwa kazi wanayoifanya kwenye kampeni huku akitoa wito kwa jeshi hilo kuendelea kukemea vitendo vya udhalilishaji kwa wanawake.

 

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi