China yapitisha sheria kuwaadhibu watu wanaoipuuza bendera ya taifa


 Bunge la China leo limepitisha mabadiliko ya sheria yanayofanya kuwa jinai kitendo cha kuidharau kwa makusudi bendera na nembo ya taifa baada ya waandamanaji wanaoipinga serikali mjini Hong Kong kuifuja na kunajisi bendera ya China. 

Kulingana na sheria hiyo mpya itakayoanza kutumika Januari mosi mwaka unaokuja, wote watakaochoma, kuichana, kuitia rangi au kuikanyaga bendera na nembo ya taifa hadharani watachunguzwa kwa makosa ya jinai. 

Sheria hiyo pia inaeleza kuwa bendera ya taifa haiwezi kupuuzwa, kupeperushwa juu chini au kutumika kwa njia zozote zinatakazoshusha hadhi ya alama hiyo ya taifa. 

Mwaka uliopita watu watatu walihukumiwa kifungo gerezani baada ya China kukasirishwa na kitendo cha waandamanaji mjini Hongkong kufanya vitendo vya dharau ikiwemo kuikanyaga bendera ya taifa.


Post a Comment

0 Comments