Kansela Merkel atoa wito kwa wajerumani kuungana na kudhibiti janga la corona

 


Kansela wa Ujerumani bibi Angela Merkel leo amewatolea wito raia wa nchi hiyo kushirikiana pamoja kupunguza kusambaa kwa virusi vya corona katika wakati Ujerumani imetangaza idadi kubwa ya maambukizi ya siku ya COVID-19. 

Kupitia ujumbe wa kila wiki wa video bibi Merkel amesema hatma ya maisha ya kawaida kwa raia wa nchi hiyo kuelekea majira ya baridi na sikukuu za mwisho wa mwaka itategemeana na mwenendo wa tabia za watu. 

Mapema leo Ujerumani ililiripoti visa vipya 7,830 vya maambukizi ya virusi vya corona katika muda wa saa 24 zilizopita, idadi ambayo ndiyo kubwa zaidi kuwahi kurikodiwa kwa siku moja tangu kuanza kwa janga la COVID-19. 

Mataifa mengine ya Ulaya yameendelea kurejesha marufuku za kupambana na virusi vya Corona, ikiwamo Ufaransa ambayo leo inaanza kutekeleza amri ya kutotoka nje usiku kwenye mji mkuu Paris, na miji mingine 8 iliyo mikubwa.


Post a Comment

0 Comments