F Shule ya St Augustine yaongoza Hanang', yaibuka ya tatu mkoani Manyara. | Muungwana BLOG

Shule ya St Augustine yaongoza Hanang', yaibuka ya tatu mkoani Manyara.


Na John Walter-Manyara

Shule ya Kanisa Katoliki Parokia ya Katesh, St. Augustine English Medium School, imeandika historia mpya baada ya kuibuka nafasi ya kwanza katika Wilaya ya Hanang’ na nafasi ya tatu katika Mkoa wa Manyara kwa matokeo ya hivi karibuni ya kitaaluma.


Mafanikio hayo yameifanya shule hiyo kuwa miongoni mwa shule bora zaidi mkoani Manyara, jambo linaloonesha juhudi kubwa za walimu, wanafunzi pamoja na uongozi wa shule na kanisa kwa ujumla.

St. Augustine imepata wastani wa alama 269.05, na hivyo kuthibitisha ubora wake katika utoaji wa elimu yenye misingi ya taaluma na maadili.

Kwa upande wa mkoa wa Manyara, shule kadhaa zimefanikiwa kuingia katika orodha ya shule kumi bora, zikionesha ushindani mzuri na kuimarika kwa sekta ya elimu katika mkoa huo.

Shule hizo na wastani wa alama zao ni kama ifuatavyo:

DEIRA – 276.73 (Babati Mji)

MERERANI ADVENTIST – 271.47 (Simanjiro)

ST. AUGUSTINE – 269.05 (Hanang’)

SIDAY – 264.45 (Mbulu Mji)

DEBORA – 261.45 (Babati Mji)

MORIAH PARADISE – 260.46 (Hanang’)

MT. HANANG – 259.98 (Hanang’)

KING’S MODERN – 255.32 (Babati DC)

ST. JOSEPH – 252.62 (Hanang’)

ST. CLARE OF ASSISI – 248.98 (Babati Mji)

Mafanikio haya yanaonesha wazi kuwa Mkoa wa Manyara unaendelea kupiga hatua katika kuboresha elimu, huku Wilaya ya Hanang’ ikijivunia kuwa na shule kadhaa zilizofanya vizuri, ikiwemo St. Augustine, Moriah Paradise, Mt. Hanang na St. Joseph.

Wadau wa elimu wamepongeza jitihada hizi na kutoa wito kwa shule nyingine kuendelea kuwekeza katika ubora wa ufundishaji, nidhamu na mazingira bora ya kujifunzia ili kuongeza ushindani chanya na kuinua kiwango cha elimu kwa ujumla.


Chapisha Maoni

0 Maoni