Jeshi la Ulinzi wa Wananchi
wa Tanzania JWTZ limekanusha taarifa zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii
yenye maudhui ya maandamano yenye lengo la kuwahadaa wananchi na kusababisha
vurugu na kubainisha kuwa taarifa hizo si za kweli na hazijatolewa na JWTZ huku
likitoa onyo kali kwa wanaojihusisha na vitendo hivyo.
Katika taarifa kwa umma
iliyotolewa na Jeshi hilo imesema Jeshi la Ulinzi wa Wananchi wa Tanzania JWTZ
linauarifu umma wa watanzania kuwa kuna tangazo linaloonekana likisambaa
mitandaoni lenye maudhui ya maandanamo kuwa ni uzushi wenye lengo la kuwahadaa
wananchi na kusababisha vurugu na uvunjifu wa amani nchini hivyo taarifa hizo
zipuuzwe.
Taarifa hiyo imekemea
tabia inayokithiri ya matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii inayolihusisha
jeshi na siasa kwa lengo la kupotosha umma na kuzua taharuki.
Taarifa hiyo imeendelea
kusema kuwa JWTZ litaendelea kushirikiana na vyombo vingine vya usalama na
mamlaka ya mawasiliano Tanzania kuwabaini na kuwachukuria hatua za kisheria
wote wanaojihusisha na upotoshaji huo.

0 Maoni