Na Amiri Kilagalila,Njombe
Waandishi wa habari nchini wametakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia usalama ili kuepuka matatizo yanayoweza kutokea katika majukumu yao ya kila siku.
Wito huo umetolewa na wakufunzi kutoka Chama cha wafanyakazi wa vyombo vya habari Tanzania (JOWUTA) wakati wakitoa semina kwa wanahabari katika ukumbi wa Dosmeza mjini Njombe juu ya maswala ya Jinsia na usalama mahala pa kazi.
Sophia Ngalapi ambaye ni mkufunzi kutoka Chama cha wafanyakazi wa vyombo vya habari Tanzania (JOWUTA) akitoa mafunzo ya jinsia na namna wanahabari wanavyotakiwa kufanya habari zinazohusu jinsia