Marekani na Brazil zinapaswa kupunguza utegemezi wa bidhaa za China - Pompeo


Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Mike Pompeo ameonya jana kuwa Marekani na Brazil zinapaswa kupunguza utegemezi wake wa bidhaa kutoka China kwa ajili ya usalama wao wakati nchi hizo mbili zikiimarisha ushirikiano wao kibiashara. 

Katika mkutano muhimu kuhusu ongezeko la ushirikiano kati ya Marekani na Brazil lenye lengo la kufufua uchumi baada ya janga la virusi vya corona, Pompeo amesisitiza umuhimu wa kupanua mahusiano ya kiuchumi baina ya nchi hizo, kutokana na kile alichokiita hatari kubwa kutokana na ushiriki wa kiasi kikubwa wa China katika uchumi wa nchi hizo. 

Msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni ya China Zhao Lijian amepinga matamshi hayo ya Pompeo.Utawala wa Trump unajitahidi kuongeza mahusiano na Brazil na kutoa nguvu mpya itakayopambana na China, ambayo inataka kupata fursa katika kile inachokiona kuwa ni ushindani mkubwa wa kuwania udhibiti wa nguvu duniani.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi