Rais wa zamani wa Bolivia aliye uhamishoni Evo Morales ameashiria nia yake ya kurudi Bolivia baada ya mgombea wa chama chake Luis Arce kushinda uchaguzi wa urais.
Arce, waziri wa zamani wa uchumi chini ya uongozi wa Morales, alidai ushindi katika uchaguzi wa Jumapili baada ya kura za maoni ya raia kuashiria ushindi dhidi ya mpinzani wake Carlos Mesa.
Matokeo hayo yamempa Arce asilimia 52 ya kura, na Mesa imepata asilimia 31.5 tu. Aidha kutokana na matokeo hayo kunatabiriwa duru ya pili ya uchaguzi huo mnamo mwezi Novemba.
Arce, mwenye umri wa miaka 57, amesema ushindi wake utakuwa ndiyo chanzo cha urudi kwa demokrasia katika taifa hilo iliyogawanyika la Amerika Kusini.
