https://monetag.com/?ref_id=TTIb Tetesi za soka kimataifa | Muungwana BLOG

Tetesi za soka kimataifa


Manchester United imeweka mipango ya kumsainisha kiungo wa Rennes na Ufaransa Eduardo Camavinga, 17, iwapo mfaransa mwenzie Paul Pogba, 27, ataamua kuondoka Old Trafford. (Sport Witness)

Uhamisho wa mshambuliaji wa Algeria Said Benrahma wa £25m kutoka Brentford kwenda West Ham uko hatarini kuvunjika, ambapo wapiga nyundo hao wamejielekeza zaidi kwa mshambuliaji wa Bournemouth raia wa Norway Josh King, 28. Crystal Palace huenda ikapeleka ofa ya lala salama kumnasa Benrahma, 25. (Mirror)

Manchester City itajaribu tena kumsajili mlinzi wa kushoto wa Ajax na Argentina Nicolas Tagliafico, 28, mwezi January. (Sun)

Tottenham huenda ikarejesha nia yake ya kumsajili mlinzi wa kati wa Inter Milan na Slovakia Milan Skriniar, 25, mwezi January. (Team Talk)

Fulham wako katika hatua nzuri ya mazungumzo ya kumsajili mlinzi wa Huddersfield na Uholanzi Terence Kongolo, 26. (Football Insider)

Wachezaji kadhaa wa Manchester United wameeleza masikitiko yao ya namna hali inavyomwendea mlinda mlango wa timu hiyo muargentina Sergio Romero, 33, ambaye amekosa nafasi Old Trafford baada ya kurejea kwa Dean Henderson, lakini uhamisho wake wa siku ya mwisho kushindikana kufuatia ada iliyowekwa ya £10m. (ESPN)

Baba wa kiungo wa Arsenal na Ghana Thomas Partey amesema kwamba mtoto wake alikuwa anasubiri timu kubwa imfuate licha ya Juventus na Chelsea kuonyesha nia ya kumtaka. (Mirror)

Kiungo wa zamani wa kimataifa wa Ujerumani anayechezea Arsenal Mesut Ozil, 31, ambaye hajacheza kikosi cha kwanza tangu mwezi Machi, mwishoni mwa Septemba alilipwa marupurupu ya mrahaba yanayofikia £8m. (The Athletic - subscription required)

Beki mfaransa Frederic Guilbert, 25, ameapa kupambania nafasi yake ndani ya Aston Villa baada ya uhamisho wake kuelekea Nantes kukwama kwenye dirisha la usajili la majira ya joto. (Express and Star)

Mshambuliaji wa zamani wa Manchester City na Brazil Robinho, 36, amejitolea kupokea mshahara wa £200 tu kwa mwezi akirejea kwa awamu ya nne kwenye klabu yake ya utotoni Santos. (Manchester Evening News)

Mtendaji mkuu wa Portsmouth Mark Catlin amesisitiza kwamba kutakuwa na wachezaji wapya Fratton Park kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili Ijumaa. (The News)

Post a Comment

0 Comments