Loading...

Oct 15, 2020

Ulaya yakabiliwa na wimbi jipya la maambukizi ya corona

 


Hofu imeongezeka leo kuwa Ulaya inapoteza fursa za kuudhibiti mripuko wa virusi vya corona katika kipindi hiki cha vuli, wakati maambukizi yanayorekodiwa kwa siku yakifika kiwango cha juu zaidi nchini Ujerumani, Jamhuri ya Czech, Ubelgiji, Uhispania, Uholanzi, Italia na Poland. 


Ufaransa imetangaza amri ya kutotembea nje kuanzia saa tatu usiku katika miji yake mikubwa. Nao wakaazi wa London wakikabiliwa na vizuizi vipya vya kusafiri wakati serikali zikiweka kanuni mpya kali.

 Mkuu wa ofisi ya Ulaya ya Shirika la Afya Ulimwenguni, WHO Dokta Hans Kluge amezihimiza serikali kutolegeza msimamo katika kudhibiti virusi hivyo. Mataifa ya Ulaya kwa pamoja yamethibitisha karibu vifo 230,000 vinavyotokana na janga la corona.

KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger