Na Timothy Itembe Mara.
Shirika lisilo la kiserikali (NG'O)la Wazee wa Tarime lililoanzishwa mwaka 2001 na kusajiliwa mwaka 2004 na hatimaye kupata hati ya ukubaliwa (Certificate of compliance) mwaka 2006.
Lengo la shirika hili ni kujenga jamii yenye kutambua na kulinda haki za msingi za Wazee kwa umoja wa watu wake kuleta Amani upendo na umoja Tarime kwa maendeleo ya wanatarime.
Simon Mnyoro alisema kuwa shirika lake linaomba jengo la makumbusho alisema hayo mbele ya Jonadhan Machango ambaye ni Afisa Tarafa Inchage ambaye alimwakilisha mkuu wa wilaya Mtemi Msafiri.
Maadhimisho ya siku ya wazee duniani huadhimishwa na kusherehekewa 01,10 kila mwaka ambayo kwa Tarime yalifanyika jana kwenye ukumbi wa Chuo cha uuguzi Tarim(NTC) na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa wilaya na mkoa Mara.
"Kupitia Ofisi yako wazee tunaomba kupata kuwepo jengo la makumbusho ya jamii yetu ambamo kutakuwemo na kumbukumbu mbali za kijamii za mkoa Mara (Historya) kwa kuzingatia kuwa mwaasisi wa Taifa hili Marehemu Julius Kambarage Nyerere alitoka Mara"alisema Mnyoro.
Mnyoro alitumia nafasi hiyo kushukuru serikali kuwakumbuka wazee na kuwatengea dirisha lao kwa ajili ya matibabu sasa kinacho hitajika nikuboreshwa huduma yenyewe,madwa yawepo badala ya wazee kuwambiwa kwenda kujinunulia kwenye vibanda vya watu binafsi hali hawana kipato.
Akikabidhi kwa wazee baadhi vitambulisho vya matibabu kwa wazee,Jonadhan Machango aliwataka Wazee kutumia vitambulisho hivyo kwa manufaa ya matibabu kulingana na sera inavyotamka.
