Bunge la Afghanistan lawaidhinisha wabunge 10


Ikiwa ni zaidi ya mwaka mmoja baada ya kufanyika kwa uchaguzi tata wa rais, bunge la Afghanistan limeidhinisha majina 10 ya mawaziri muhimu nchini humo. 


Miongoni mwa mawaziri walioidhinishwa ni pamoja na waziri wa ulinzi, uhusiano ya nje na waziri wa mambo ya ndani. Zoezi hilo la upigaji kura la leo hii linafanyika katika kipindi ambacho mji wa Kabul, umeshambuliwa kwa maroketi 23, ambayo yamesababisha vifo vya watu 8 na wengine 21 kujeruhiwa. 


Mwezi Oktoba, Rais, Asharf Ghani alitangaza tu pendekezo la baraza la mawaziri 26, baada ya kuwepo mvutano wa kisiasa na hasimu wake, Abdullah Abdullah. 


Katika siku kadhaa zijazo idadi nyingine ya wateule 13 iliyosalia itaalikwa bungeni kujitambulisha na kuelezea mipango yao. 


Idadi kubwa ya mawaziri iliyoshinda mchakato huo wa kupigiwa kura ni wale waliotambulishwa na washirika wa kisiasa wa Abdullah, ambae ni mkuu wa Baraza la Upatanishi la Kitaifa la Afghanistan.

Post a Comment

0 Comments