.

.

Jun 19, 2021

Clippers yatamba NBA na kuweka rekodi yake mpya

  Muungwana Blog       Jun 19, 2021


Los Angels Clippers imeinyuka Utah Jazz kwa alama 131-119 na kusonga mbele hadi hatua ya fainali kanda ya magharibi kwa mara ya kwanza kwa ushidni wa michezo 4-2 .


Terance Mann aliifungia Clippers ambao walikuwa nyuma kwa alama 25 katika robo ya tatu ya mchezo huo huku Paul George akifunga alama 28 na kucheza mipira ya kurudi mara 9 na assisti 7 akichagiza ushindi huo.


Ikumbukwe Clipers wameshinda mchezo huo bila ya uwepo wa nyota wao Kawhi Leonard ambaye kwa sasa ni majeruhi.


Katika fainali Los Angeles Clippers itakipiga dhidi ya Phoenix Suns.


Katika kanda ya Mashariki, Phidalelphia 76ers wamelazimisha sare ya 3-3 na Atalanta Hawks baada ya ushindi wa leo hivyo watacheza mchezo wa saba ili kupata mshindi.

logoblog

Thanks for reading Clippers yatamba NBA na kuweka rekodi yake mpya

Previous
« Prev Post

No comments:

Post a Comment