Waziri wa Ulinzi wa Uingereza Ben Wallace ameonyesha wasiwasi wake juu ya kuendelea kwa machafuko nchini Afghanistan, akisema nchi hiyo inaelekea kuwa taifa lililosambaratika kisiasa na kiuchumi.
Wallace
amesema nchi hiyo inaweza kugeuka na kuwa uwanja wa kulea makundi ya
kigaidi kama al-Qaeda, na kuonya kuwa kundi hilo linaweza kuibuka
upya.Waziri huyo wa Ulinzi ameongeza kusema kuwa mataifa ya Magharibi
yanafaa kuelewa kwamba hayawezi papo kwa hapo kusuluhisha matatizo
katika mataifa kama vile Afghanistan.
Kasi ya kundi la Taliban la
kuyakamata miji mikuu ya mikoa muhimu nchini Afghanistan imeitia
wasiwasi serikali ya mjini Kabul na washirika wake wa magharibi
wakiongozwa na Marekani, ambao wameondoa vikosi vyao vya ulinzi.
