Kamati ya bunge ya Brazil imesema Rais Jair Bolsonaro anapaswa kushitakiwa kwa makosa tisa ya uhalifu yenye kuhusiana na namna taifa hilo lilivyoshughulikia janga la virusi vya corona,yakiwemo ya ulaghai na uhalifu dhidi ya binaadamu.
Seneta Renan Calheiros jana jioni
aliwasilisha ripoti ya mwishio iliyohusu sera ya serikali ya Bolsonaro
katika kuabiliana na janga la virusi vya corona baada ya uchunguzi
uliodumu kwa miezi sita. Hata hivyo kinakachofauta baada ya hatua hiyo
bado hakijawa wazi.
Aidha ripoti hiyo imesema kando na Bolsonaro, watu
wengine 65 wakiwemo wafanyabiashara wawili pia wanapaswa kukabiliwa na
mashtaka.
Bolsonaro amekuwa akipuuza athari za virusi vya corona tangu
kuanza kwa janga hilo na alikuwa akipinga hatua za kujikinga na kuonesha
mashaka na matumizi ya chanjo. Amekuwa akisisitiza mara kadhaa kwamba
hata chanjo hajashiriki.
0 Comments