Urusi yaialika Taliban kwa mazungumzo kufuatia kitisho cha IS

 


Urusi imelialika kundi la Taliban kwa mazungumzo mjini Moscow leo Jumatano, ikinuia kupanua ushawishi wake katika eneo la Asia ya kati na kushinikiza hatua dhidi ya kundi linalojiita Dola la Kiislamu ambalo linalaumiwa kufanya mashambulizi nchini Afghanistan. 

Mazungumzo hayo yanayohusisha maafisa kutoka mataifa 10 ikiwemo China na Pakistan, ni miongoni mwa mashauriano muhimu ya kimataifa tangu kundi la Taliban lilipoingia madarakani mwezi Agosti nchini Afghanistan. 

Mazungumzo hayo yanakuja baada ya Rais wa Urusi Vladimir Putin kuonya wiki iliyopita kuwa wapiganaji wa IS wanajikusanya nchini Afghanistan ili kufanya mashambulizi kwenye mataifa ya uliokuwa muungano wa kisovieti Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov anatarajiwa kuhutubia mkutano huo wakati ujumbe wa Taliban ukiongozwa na naibu waziri mkuu Abdul Salam Hanafi, afisa mwandamizi katika utawala wa Afghanistan ambaye pia alifanya mazungumzo na Umoja wa Ulaya na Marekani wiki iliyopita.


Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi