Ethiopia yasema uhusiano wake na Marekani uko hatarini


Ethiopia imeituhumu Marekani kwa kusambaza habari za uwongo kuhusu hali ya usalama katika taifa hilo linalokumbwa na vita, huku ikionya kuwa habari kama hizo huenda zikatia doa uhusiano wa mataifa hayo mawili. 


Marekani iliwahi kuizingatia Ethiopia kama mshirika muhimu wa usalama katika eneo la pembe ya Afrika lakini uhusiano wa mataifa hayo mawili umeanza kuyumba, kufuatia mgogoro wa zaidi ya mwaka mmoja nchini Ethiopia dhidi ya waasi ambao wametishia kusonga mbele kuingia Addis Ababa. 


Tarehe 5 Novemba, Marekani iliwaondoa wafanyakazi wa ubalozi wake mjini humo kufuatia hali ya usalama kuwa mbaya. 


Wiki hii ubalozi wa Marekani uliukasirisha zaidi utawala wa Abiy Ahmed kwa kutoa onyo juu ya uwezekano wa shambulio la kigaidi kutokea Ethiopia. Msemaji wa serikali Kebede Desisa amesema matamshi ya Marekani yanaumiza pande zote na huenda yakauharibu vibaya uhusiano wao.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi