RC Rubirya ashindwa kuridhishwa na hali ya matengenezo ya barabara Njombe


Na Amiri Kilagalila,Njombe

Mkuu wa mkoa wa Njombe Mhandis Marwa Rubirya amewataka wahandisi wa TANROADS na TARURA kukamilisha taratibu za manunuzi ili kutengeneza barabara zilizopo kwenye halmashauri kwa wakati.


Mhandisi  Rubirya amesema hali ya matengenezo hairidhishi na kuagiza Tanroads na Tarula kuanza mapema  mchakato wa manunuzi kabla mvua hazijaanza.


Mkuu wa mkoa  wa  Njombe Mhandis  Rubirya ametoa kauli hiyo akiwa katika  kikao cha bodi ya barabara kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya mji wa Njombe na kutaka kila mwananchi kuwa mlinzi wa miundombinu ya barabara.


“Tunaelekea mwishoni mwa mwezi wa kumi na moja lakini bado haliridhishi lakini kama mvua ingeanza kunysha hali ingekuwa ni mbaya zaidi kwa hiyo ni lazima mbadilike,mchakato wa manunuzi uanze mapema ili wandarasi wapatikane kwa wakati na hatimaye matengenezo yaanze kabla ya msimu wa mvua”alisema Rubirya


Baadhi ya wajumbe wa kikao cha bodi ya barabara akiwemo mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Bwana Valentino hongoli na mbunge wa makambako Deo Sanga  wametaka serikali kuharakisha matengenezo ya barabara ya Kibena Madeke  hadi Mlimba  kwa kiwango cha lami.


“Lakini kuhusu barabara ya Kibena-Lupembe ushauri wangu kwasababu kuna fedha ambazo zilishatengwa tungeanza hata kama hela ni kidogo”alisema Deo Sanga Mbunge wa Makambako


Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Mkoa wa  Njombe Bwana Jasel Mwamwala amesema barabara ya Kibena Madeke  hadi mlimba inatakiwa kutiliwa mkazo kwani kisiasa italeta athali kwa chama.


“Katika kikao kilichopita tulionyesha kwamba barabara hii ya Njombe-Lupembe inaweza ikatughalimu tulieleza kabisa ianze kujengwa na tukizungumzia kisiasa tutapata shida kweli kweli uchaguzi ukija kwasababu tuliahidi,mimi nafikiri hebu tutizame ili tusijekuathirika”alisema Mwamwala.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi