Na Baraka Messa, Songwe
MKUU wa Mkoa wa Songwe Omary Mgumba ametangaza kuwakamata wanaowafanyia ukatili wanawake wajawazito kwa kuwapeleka kujifungulia kwa wakunga wa jadi badala ya hospitalin na kupelekea vifo vya mama na mtoto.
Alisema hayo kwenye ziara yake katika wilaya ya Mbozi wakati akiongea na Wananchi na kukagua ujenzi wa kituo Cha afya Nambinzo.
Alisema pamoja na Serikali kujenga na kuboresha Huduma za afya kwa kuwasogezea zahanati, vituo vya afya , hospital za Wilaya na mkoa kuwa bado kuna jamii mkoani Songwe inawapeleka wanawake kwa wakunga wa jadi na kuhatarisha maisha ya mama na mtoto wakati wa kujifungua.
" Tukimkuta mke wako kwa mama Ngojea (mkunga wa jadi) tunakuchukua wewe baba na tunakupeleka gerezan ukamngojee mke wako huko, alafu tunamchukua mke wako tunampeleka hospitalini ili kuokoa uhai wake na mtoto,
Akijifungua naye tunamsubiri siku 40 ataungana na wewe gerezani ili muendelee kungojea vizur" alisema Mgumba.
Alisema kitendo Cha baadhi ya wanaume kuwafanyia ukatili kuwapeleka kwa wakunga wa jadi wake zao ni chanzo Cha kutokea vifo vya mama na mtoto kwa Mkoa wa Songwe.
Mganga Mkuu mkoa wa Songwe Nyembea Hamad alisema licha ya Mkoa wa Songwe kufikiwa na vituo vya afya 214 vinavyofanya kazi kuwa bado kuna changamoto ya wanawake wanapelekwa kujifungulia kwa wakunga wa jadi.
Alisema maeneo yaliyokithiri ukatili huo kuwa ni pamoja na kata ya Itaka kwa upande wa wilyaya ya Mbozi, kata ya mkomba Wilaya ya Momba, Wilaya ya Songwe na Ileje.
"Tunaendelea kutoa elimu kwa kuwapa elimu Viongozi wa vijiji na kuwasihi kutoa taarifa pindi matukio hayo yanapotokea maeneo yao, pia Viongozi wengi wa Serikali wanapokuwa kwenye Majukumu yao kukutana na Wananchi wanayakemea kitendo hicho" alisema Nyembea.
Alisema jamii inatakiwa kubadilika kutokana na madhara makubwa yanayowapata wanawake ikiwa ni pamoja na kupoteza uhai wa mtoto au yeye mwenyewe kufariki.
Alisema jamii ya zamani ilitumia njia hiyo kutokana na kutokuwepo Huduma za kiafya kabisa.