Taarifa kutoka Ikulu ya Urusi imesema rais wa taifa hilo Vladimir Putin amemfuta kazi mkuu wa huduma za magereza baada ya mikanda ya vidio kuonyesha picha za kuogofya za mateso na matukio ya ubakaji.
Putin amemsimamisha kazi mara moja Alexander Kalashnikov aliyelengwa katika vikwazo vya Magharibi kufuatia kufungwa kwa mkosoaji wa serikali ya Alexei Navalny.
Nafasi ya Kalashnikov aliyehudumu kama mkuu wa magereza kwa miaka miwili, imechukuliwa na Arkady Gostev kanali kutoka wizara ya ndani ya Urusi.
Hatua hiyo inatokana na makundi ya kutetea haki za binaadamu mwezi uliopita kuchapisha video zinazoonyesha mateso ndani ya gereza moja mjini Saratov.
Vidio hizo zilitolewa na Sergei Savelyev aliyewahi kuwa mfungwa katika gereza hilo ambaye kwa sasa ameitoroka nchi na kuomba hifadhi nchini Ufaransa.