Wanachama watano wa bunge la wawakilishi nchini Marekani wanatarajiwa kuwasili Taiwan hapo kesho Ijumaa, kwa ziara fupi itakayowakutanisha na waziri wa ulinzi wa kisiwa hicho, hii ikiwa ni kulingana na vyombo vya habari vya Taiwan.
Ziara hiyo inakuja wakati China ikiwa imeendeleza shinikizo za kijeshi na kisiasa kuendelea kudai umiliki wa kisiwa hicho, hatua inayozidisha hasira Taiwan ambako serikali imeapa kutetea uhuru na demokrasia yake. Ujumbe huo wa Marekani pia utakutana na rais wa Taiwan Tsai Ing-wen.
Hata hivyo wizara ya kigeni na ile ya ulinzi zimekataa kutoa maelezo zaidi kuhusiana na ujio wa wabunge hao wa Marekani.