Maelfu ya waandamanaji Sudan wamekusanyika katika mji mkuu Khartoum kupinga mapinduzi ya kijeshi na kukataa makubaliano yaliopatikana kati ya jenerali mkuu wa jeshi Abdel Fattah al-Burhan yaliomfanya waziri Mkuu Abdalla Hamdok kurejeshwa katika nafasi yake.
Mjini Khartoum waandamanaji walisema kwa sauti "watu wanataka kuanguka kwa utawala uliopo" huku katika miji mingine kama Om-durman wengine walisema pia kwa sauti "nguvu kwa umma, utawala wa kiraia ndio matakwa ya watu wa Sudan"Jenerali Abdel Fattah al-Burhan aliongoza mapinduzi ya kijeshi na kuchukua madaraka, kumkamata Waziri Mkuu Abdalla Hamdok tarehe 25 mwezi Oktoba lakini baada ya ulimwengu wa kimataifa kuikosoa hatua hiyo na maandamano makubwa dhidi ya jeshi kupinga mapinduzi, siku ya Jumapili alimrejesha katika nafasi yake Waziri Mkuu Hamdok.
Waandalizi wa maandamano katika taifa hilo la Kaskazini Mashariki mwa Afrika wamemtuhumu Hamdok kwa usaliti na kuapa kuendelea kutoa shinikzo kwa jeshi kurejesha uongozi kamili kwa utawala wa kiraia.