Tume yataka mashtaka dhidi ya zama za Jammeh Gambia


Tume ya Ukweli na Maridhiano ya Gambia, TRRC, jana Alhamisi imewasilisha ripoti yake kwa kupendekeza maafisa waliohusika na uhalifu uliotendwa chini ya uongozi wa kiongozi wa zamani, Yahya Jammeh, wafunguliwe mashitaka huku wahanga wakisisitiza kwamba kiongozi huyo wa zamani mwenyewe lazima ajumuishwe kwenye mashitaka hayo.


Tume hiyo TRRC imekabidhi ripoti yake ya uchunguzi kwa Rais Adama Barrow na kutoa pendekezo la serikali kuendelea na mashtaka ya uhalifu.Mwenyekikiti wa TRRC Lamin Sise amesema ripoti imewataja kwa majina wale wote waliotwishwa mzigo mkubwa wa tuhuma za ukiukwaji wa haki za binaadamu na unyanyasaji. 


Kwa muda mrefu makundi ya haki za binaadamu yamekuwa yakipiga kelele kwamba Jammeh ashitakiwe kwa tuhuma za mauwaji, mateso na ubakaji katika kipindi cha miaka 22 ya utawala wake.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi