Wataalam imeonya kuwepo kwa uperesheni tata za kinu chake cha nyuklia

 


Korea Kaskazini inaendeleza shughuli zake tata katika kinu chake cha nyuklia cha Yongbyon, hatua ambayo wataalamu wanasema inatoa uwezekano wa uundwaji wa mabomu ya nyuklia. 


Wachambuzi ambao wanafanyia tovuti ya habari iiitwayo "38 North", ambayo inaendeshwa na asasi ya Kimarekani ambayo imejikita katika masuala ya Korea Kaskazini, Stimson Center inasema picha za taswira za setilaiti katika majuma ya hivi karibuni zinaonesha ushahidi zaidi kwamba kinu hicho kinafanya kazi.


Mapema Agosti Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki (IAEA) lilisema zipo ishara kwamba Korea Kaskazini imeanza tena shughuli za kinu hicho tangu Julai 2021.


Pasipo kutoa ufafanuzi zaidi, tovuti 38 North, imenukuu taarifa ya msemaji wa Wizara ya Muungano Korea Kusini pamoja na Marekani, ikisema wataendelea kufuatilia mwenendo wa Korea Kaskazini kwa karibu.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi