Ecowas yaonya wanajeshi wa Burkina Faso kuhusu jaribio la mapinduzi

Majirani wa Burkina Faso wanasema wanawalaumu wanajeshi waasi wanaohusika kuzuiliwa kwa Rais Roch Kaboré.

Jumuiya ya kiuchumi ya mataifa ya Afrika magharibi ECOWAS imetaja matukio ya Jumapili na Jumatatu kuwa "jaribio la mapinduzia" - pamoja na kuripotiwa kumkamata rais, wanajeshi wamechukua kituo cha utangazaji cha serikali RTB.

Wanaohusika na uasi huo wanataka mabadiliko katika uongozi wa jeshi na raslimali zaidi katika juhudi za kupigana na wanamgambo wa kijihadi.

Bado haijabanika ikiwa ujumbe uliochapishwa kwenye akaunti ya Twitter ya Bw Kaboré siku ya Jumatatu, unaotaka demokrasia ya nchi hiyo kulindwa ulitoka kwa rais mwenyewe. Hajaonekana hadharani tangu ripoti za kuzuiliwa kwake kuibuka.

Jumuiya hiyo yenye wanachama 15 imesimamisha uanachama wa Mali na Guinea na kuziwekea vikwazo baada ya wanajeshi katika nchi hizo mbili kunyakua mamlaka.

 

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi