Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch linataka uwazi kutoka kwa serikali ya Burundi kuhusu moto wa magereza ambao uliua makumi ya watu mwezi Disemba mwaka jana.
Takriban watu 38 walikufa, na wengine wengi kujeruhiwa moto ulipozuka katika gereza la Gitega, jengo lililojengwa kuhifadhi wafungwa 400, ambalo lilikuwa na zaidi ya wafungwa 1,500 wakati huo.
Ripoti ya HRW iliyotolewa, inasema kwamba huku serikali ikidai kwamba idadi ya waliofariki ni chini ya watu 50, akaunti za wafungwa zinapinga na kusema waliofariki ni kati ya 200 na 400.
Ripoti hiyo inaongezea kuwa vyanzo vya magereza vilivyokuwepo wakati miili hiyo inatolewa vilishuhudia miili ikisafirishwa ndani ya mifuko mikubwa ya plastiki, mingine ikiwa na miili mingi.
Pia inadai kwamba mabaki mengine yalizikwa ‘katika makaburi ya halaiki jioni ya Desemba 7 bila juhudi zozote za kuwatambua.
Ripoti hiyo inaomba hisabu sahihi ya idadi ya watu waliofariki, yakiwemo majina yao, na yeyote anayehusika na tukio hilo achukuliwe hatua.