Urusi inapanga "kura ya maoni" katika mji wa kusini wa Kherson kwa lengo la kuhalalisha kuuteka mji huo , kulingana na ripoti ya hivi punde ya Wizara ya Ulinzi ya Uingereza.
Inasema kuwa jiji hilo ni muhimu kwa lengo la Urusi la kuanzisha daraja la ardhini kuelekea peninsula ya Crimea - ambayo ilitwaliwa na Urusi mwaka 2014 - na kutawala kusini mwa Ukraine.
Inaongeza kuwa Urusi ilitumia mbinu hii ili kuhalalisha unyakuzi wake wa Crimea.
Kherson ndio mji mkuu pekee ambao Urusi imeweza kuuteka tangu ilipovamiaUkraine mwishonimwa mwezi Februari. Lakini baadhi ya maeneo jirani yamechukuliwa tena na wanajeshi wa Ukraine, na mapigano katika eneo hilo yanaendelea.
