Afrika Kusini yathibitisha tena kujitolea kuitaifisha benki kuu


Chama tawala cha African National Congress nchini Afrika Kusini kimethibitisha msimamo wake kwamba benki kuu nchini humo inapaswa kutaifishwa. 


Rais wa nchi hiyo Cyril Ramaphosa amesema hayo leo baada ya uamuzi huo kufanywa wakati wa kongamano la sera siku tatu zilizopita.Katika hotuba yake ya kuhitimisha, Ramaphosa amesema kuwa kongamano hilo lilitaja kasoro hiyo ya kihistoria ya kubinafsishwa kwa benki hiyo kuu na kuthibitisha tena azimio kwamba benki hiyo inapaswa kumilikiwa kikamilifu na raia wa Afrika Kusini. 


Ramaphosa ameongeza kuwa wajumbe katika kongamano hilo walikuwa wameihimiza serikali kufanya hivyo kwa njia na kasi ambayo ingezingatia gharama kwa hazina ya taifa hilo ambayo tayari imetumika kwa kiwango kikubwa. 


Tofauti na benki kuu nyingi duniani, benki kuu ya Afrika Kusini inamilikiwa na watu binafsi. Mnamo mwaka 2017, chama cha ANC kiliazimia kuitaifisha kikamilifu lakini bado hakijatekeleza uamuzi huo.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi