Ticker

6/recent/ticker-posts

Zelensky awaomba WaRusi kupinga tangazo la Putin la kuongeza wanajeshi


Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amewatolea mwito raia wa Urusi kuukataa mpango wa rais Vladimir Putin wa kukusanya wanajeshi zaidi kwenda vitani nchini Ukraine, tangazo lililosababisha maandamano makubwa nchini Urusi. 


Zelensky amenukuliwa akiwaambia raia wa Urusi kwamba tayari wanajeshi 55,000 wa Urusi wamekufa katika kipindi cha miezi sita ya vita, na kama hawatataka idadi kuongezeka wanatakiwa kupinga, kukimbia ama kujisalimisha dkwa jeshi la Ukraine. 


Amesema wanawake wa Urusi wanatakiwa kuamua ama kuwalinda waume, watoto na wajukuu zao ama kuwaacha wakafie kwenye vita viliyoanzishwa na Putin huku akiwaonya wanaume nao kuchagua ama kufa au kuishi na ulemavu. Zaidi ya watu 1,300 tayari wamekamatwa na polisi kote nchini Urusi wakati walipoandamana kupinga tangazo hilo.

Post a Comment

0 Comments