Ukraine: Watu waambiwa waondoke kwenye vitongoji kadhaa vya jimbo la Kherson kuepuka baridi


Idara za serikali nchini Ukraine zimeanza kuwaondoa raia kutoka kwenye baadhi ya sehemu za jimbo la Kherson zilizokombolewa hivi karibuni ili kuepuka hali mbaya iliyosababishwa na mashambulio ya Urusi. Pana hofu ya kukosekana nishati na maji. 


Shirika la afya duniani WHO limesema linakubaliana na tathmini hiyo na limetahadharisha kwamba mamilioni ya watu wanaweza kukabiliana na hali ya kuhatarisha Maisha mnamo msimu huu wa baridi kali nchini Ukraine. 


Serikali ya Ukraine inawataka raia kwenye majimbo mawili ya kusini wahamie kwenye sehemu za usalama. Majeshi ya Urusi kwa miezi kadhaa yamekuwa yanayashambulia maeneo hayo kwa mizinga.


Makamu wa waziri mkuu wa Ukraine Iryna Vereshchuk amesema serikali itaoa huduma za usafiri, malazi na za afya kwa ajili ya wananchi. Amesema watoto, wanawake, wagonjwa na wazee watapewa kipaumbele.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi