Urusi yakasirishwa na papa Francis kwa kudai vikosi vyake ni 'katili zaidi'

 


Urusi imekashifu maoni kutoka kwa Papa kwamba baadhi ya vikundi vya wanajeshi walio wachache wamekuwa na tabia mbaya zaidi kuliko wengine katika uvamizi wa Ukraine.


Wanajeshi "wakatili zaidi" kwa ujumla ni Wachechnya na Buryats, Papa Francis aliliambia jarida la Marekani.


Pia aliita njaa ya Holodomor iliyosababishwa na Kremlin nchini Ukraine katika miaka ya 1930 kuwa mauaji ya halaiki.


Urusi ilitaja matamshi hayo kuwa "upotovu", na kusema makundi ya kitaifa ni "familia moja".


Katika mahojiano na Amerika, jarida la Jesuit, Papa Francis aliulizwa juu ya kusita kwake dhahiri kushutumu Urusi moja kwa moja kwa vita.


Akijibu alisema alipata "taarifa nyingi kuhusu ukatili wa askari".


"Kwa ujumla, wakatili zaidi labda ni wale ambao ni wa Urusi lakini sio wa mila ya Kirusi, kama vile Wachechnya, Waburya na kadhalika," alisema.


Papa aliongeza kuwa "anayevamia ni taifa la Urusi".


Wachechnya, kabila linalotoka Chechnya, kusini-magharibi mwa Urusi, wengi wao ni Waislamu.


Buryats, kabila la Wamongolia wenye asili ya Buryatia, mashariki mwa Siberia, kwa kawaida hufuata mifumo ya imani ya Kibuddha na shaman.


Urusi ina jamhuri nyingi zenye vikundi tofauti vya kikabila na kidini. Dini kubwa ni Ukristo wa Orthodox.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi