https://monetag.com/?ref_id=TTIb CHADEMA YAWAONDOA HOFU POLICE MKUTANO WA MBOWE TARIME. | Muungwana BLOG
https://monetag.com/?ref_id=TTIb

CHADEMA YAWAONDOA HOFU POLICE MKUTANO WA MBOWE TARIME.


 Na Timothy Itembe Mara.


MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA  jimbo la Tarime mjini,Bashiri Selemani maarufu SAUTI amewahakikishia amani jeshi la polisi kwenye mkutano wa mwenyekiti chama hicho Taifa wilayani hapa unaotarajiwa kufanyika januari 23,2023.


Mkutano huo umepangwa kufanyika katika viwanja vya mazoezi ya mpira wa miguu Sabasaba (maarufu shamba la Bibi )uwanja uliopo mtaa wa Serengeti mkutano ambao umelenga  kueleza sera,Ilani ya chama hicho pamoja na kukosoa Serikali katika utekelezaji wa shuguli za maendeleo pale ambapo hazikufanyika kwa uwazi.


Mwenyekiti huyo alisema kuwa wananchi pamoja na vyombo vya usalama wakiwemo jeshi la polisi wanatarajia kushuhudia mkutano utakao enda kufanyika kwa amani na utulivu na wasiwe na wasiwasi mkutano na kuwa wananchi wahudhurie kusikiliza sera pamoja na ilani ya chadema.


“Ndugu zangu mikutano ya hadhara ya kisiasa inatakiwa kufanyika kwa mjibu wa katiba ya jamuhuri ya muungano ya Tanzania  lakini ilizuiliwa na sasa imefunguliwa kufanyika na wapinzani wetu CCM wasiwe na wasiwasi mikutano itaenda kufanyika kwa amani na usalama tunacho hitaji tunatakiwa kueneza sera na atakaye bainika anatoa lugha ya kashifa na matusi atawajibika mwenyewe na  chama hakitahusika”alisema Sauti.


Sauti alimaliza kwa kusema mwenyekiti Chadema Taifa,Freemani Mbowe atakuwa mgeni rasimi wa mkutano huo na ataenda kuzungumza na wazee wa Chama chake ili kubadilishana mawazo na uzoefu wa shughuli za chama na kujipanga katika uchaguzi uliopo mbele yao wa serikali za mitaa kama watashiriki.

Post a Comment

0 Comments