https://monetag.com/?ref_id=TTIb Mbunge Kembaki kugharimia mwanasheria kuchunguza kesi ya bomoa bomoa soko jipya Rebu | Muungwana BLOG
https://monetag.com/?ref_id=TTIb

Mbunge Kembaki kugharimia mwanasheria kuchunguza kesi ya bomoa bomoa soko jipya Rebu


 Na Timothy Itembe Mara.

MBUNGE wa jimbo la Tarime Mjini,Michael Kembaki kugharimia mwanasheria ili sheria sheria ya kubomolewa kesi ya wananchi wake makazini na maeneo waliokuwa wakifanyia biashara ndogondogo.

Akiongea na huku akikabidhi msaada wa chakula kwa wahanga hao katika maeneo ya mtaa wa Mkuyuni ya Turwa mjini hapa alisema licha ya kuwa ubomoaji ulifanyika chini ya utaratibu wa kisheria atahakikisha anagharimia sheria ili sheria ya kesi hiyo na wananchi wake wakapata haki.


Kembaki alionyesha kusikitishwa na kitendo hicho ambapo alisema maeneo hayo yalikuwa yakinufaisha watu wengi kwa hali hiyo waliofungua kesi na mwenendo wake walitakiwa kutumia busara hata kama kuomba fidia wafidiwe ili wananchi waendelee kuishi na kufanya shuguli badala ya kuwabomolea.


“Mimi niseme zoezi lililoendeshwa la ubomoaji siliungimkono kwa hali hiyo nitahakikisha nagharimia mwanasheria waona usahihi na mwenendo wa kesi ili wananchi wangu wakaende kupata haki na zoezi hilo naona kama linamazingira ya rushwa huwenda maofisa wa halmashauri nina mashaka wanahusika katika hili”alisema Kembaki.


Mbunge huyo alitumia siku hiyo kuwakabidhi wafanya biashara wajasilia mali wadogo wa mtaa wa mwangaza taa za sola zenye dhamani ya shilingi milioni 4 ili kufanya biashara katika maeneo ya usalama na usalama na kufanyabiashara katika maeneo yaliyoghubikwa na giza jambo ambalo ni hatari kwa biashara na mali walizonazo. .


Kwa upande wake Diwani kata ya Turwa kupitia Chama cha mapinduzi CCM,Chacha Marwa Machunbgu maarufu Chacha Musukuma alisema wapo kwenye mtaa wake na kata anayoiongoza Turwa na kuwa zoezi la ubomoaji liliendeshwa kinyamera bila yeye kujulishwa ama kuhusishwa.


Musukuma mmoja kuwa na wananchi waliobomolewa nyumba zao zikaharibiwa maeneo ya biashara wanateseka na hawana mahala pa kujihifadhi kwa hali hiyo anaomba serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassani kufikiria na kuwaonea huruma wananchi hao na kubadilisha matokeo ya hukumu na wahanga wakaendelea kunufaika na matunda ya uhuru wanchi yao.


Diwani huyo aliongeza kuwa zoezi la ubomoaji lilifanyika kwa mjibu wa sharia ya mahakama ya baraza la ardhi na nyumba ya wilaya Tarime kwa hali hiyo ambao wanatumia mwanya huo kujiimarisha kisiasa waache tabia hiyo na wasubiri wakutane kwenye majukwaa ya kisiasa na sio kupotosha wananchi.

Post a Comment

0 Comments