Netanyahu adai Iran ilijaribu kumuua mmoja wa wanawe wa kiume


Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu amedai kuwa Iran ilijaribu kumuua mmoja wa wanawe wa kiume lakini hajatoa maelezo ni lini jaribio hilo lilitokea. 

Madai ya Netanyahu yanaweka wazi wasiwasi ambao umekuwepo tangu kuzuka kwa vita kati ya Marekani- Israeli na Iran kuanza mwezi Februari, vita ambavyo vilisbaabisha kuuawa kwa kiongozi wa juu wa kiroho wa Iran Ali Khamenei na maofisa wengine wa ngazi ya juu wa serikali ya Iran.

Netanyahu, ambaye muungano wake wa kisiasa unaonekana kuwa nyuma ikwia imesalia miezi miwili kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa Oktoba 27, alitoa madai hao wakati wa mahojiano ya njia ya simu na kituo cha Habari cha Channel 14 nchini Israeli

Alikuwa akijibu ripoti kuwa moja ya vitengo vya kiusalama nchini mwake kilikataa kutoa ulinzi kwa mmoja wa wapinzani wake wa kisiasa kuelekea uchaguzi huo.

"Kwa mmoja wa wana wangu wa kiume. Hapa nadhani kuna kitu cha kustaajabisha. Ndio. Iran ilimlenga mmoja wana wangu wa kiume. Ilijaribu kumuuwa mmoja wa wana wangu," alisema Netanyahu.

"Iran ilijaribu kumuuwa mmoja wa wana wangu, na kwa hivyp hili suala la uliniz sio jambo la kistarehe.," Alisema bila ya hata hivyo kutoa ufanuzi zaidi kuhusu njama hiyo ya mauaji.

Haikuwa wazi mara moja ni yupi kati ya wanawe aliyekuwa akimzungumzia. Mwanawe mkubwa, Yair, anaishi mjini Miami nchini Marekani.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi