Na Ahmad Mmow, Nachingwea.
Chama kikuu cha ushirika cha RUNALI kilichopo mkoani Lindi, leo tarehe 18.10.2026 kimefanikiwa kuuza korosho ghafi zenye jumla ya tani 10,800,030.
Mnada huo wa kwanza kwa msimu wa 2026/2027 kwa chama hicho uliofanyika mjini Nachingwea kwenye ukumbi wa mikutano wa chama kikuu hicho . Ambapo korosho hizo za daraja la kwanza zimeuzwa kwa bei ya juu ya shilingi 3,410 Ambapo bei ya chini ni shilingi 3,270 kwa kila kilo moja.
Akitangaza matokeo ya mnada huo ulioendeshwa na soko la bidhaa Tanzania(TMX)kwa njia ya mtandao, mwenyekiti wa chama hicho, Audax Audax Mpunga alisema korosho hizo zimepatikana kutoka katika maghala makuu yote yaliyopo katika wikaya za Ruangwa, Liwale na Nachingwea. Wilaya ambazo zinaunda chama hicho.
Mpunga alisema jumla ya tani 10,800,030 zimeuzwa. Huku akibanisha kwamba katika mnada huo kulikuwa na jumla ya loti....
Aidha Mpunga alitoa wito kwa wakulima waendelee kuzingatia ubora ili wanunuzi waendelee kununua kwa bei nzuri. Kwani miongoni mwa sababu zinazochangia bei kuwa ndogo ni kukosekana kwa ubora.
Hatahivyo Mpunga aliwashukuru wakulima wa zao hilo wanaohudumiwa na chama kikuu hicho kwa kuzingatia suala la ubora. Kwani RUNALI kimekuwa ni chama ambacho korosho zake ni bora kwa misimu mingi.
Kwaupande wake mkurugenzi mkuu wa bodi ya korosho Tanzania(CBT), Fransis Alfred alitoa wito kwa wakuu wa wilaya kusaidia kufuatilia ubora wa zao hilo ili wakulima wapate bei nzuri.
Huo ni mnada wa pili kufanyika katika mkoa wa Lindi kwa msimu wa 2026/2027. Kwani mnada wa kwanza ulifanyika tarehe 17.10.2027 kupitia chama kikuu cha ushirika cha Lindi Mwambao.
