China Kuendelea Kuisaidia Nigeria Dhidi ya Ugaidi

Serikali ya China imetangaza uungaji mkono wake kwa serikali ya Nigeria katika juhudi zake za kurejesha usalama na amani nchini humo. Hayo yamesemwa na Wang Runxu, afisa wa ngazi za juu wa jeshi nchini China akiwa Nigeria na kusisitiza kuwa, China ni muungaji mkono mkubwa kwa juhudi za serikali ya Abuja katika kupambana na ugaidi. Afisa huyo wa kijeshi ameongeza kuwa, ushirikiano wa nchi yake na Nigeria katika wigo wa usalama, unazidi kuimarika.

Askari wa China wako nchini Nigeria kupitia mpango wa kutoa mafunzo kwa jeshi la nchi hiyo. Mashambulizi ya kundi la kigaidi na kitakfiri la Boko Haram, ni changamoto kuu ya usalama nchini Nigeria.


Kundi hilo lilianzisha mashambulizi yake ya kigaidi tangu mwaka 2009, na hadi sasa maelfu ya watu wameuawa na zaidi ya milioni moja kuwa wakimbizi ndani na nje ya mipaka ya taifa hilo la magharibi mwa Afrika. Mwaka huu wa 2015, kundi hilo lilipanua zaidi wigo wa mashambulizi yake hadi katika nchi za Niger, Chad na Cameroon, suala ambalo lilitoa changamoto kwa serikali ya nchi hizo kuunda muungano wa kijeshi dhidi ya kundi hilo.
Mpya zaidi Nzee zaidi