Mamlaka nchini Burundi inasema kuwa jenerali
Adolphe Nshimirimana ameuawa.
Imeripotiwa kuwa alifariki katika shambulizi la roketi
katika gari lake kaskazini
mwa mji mkuu wa Bujumbura .
Jenerali Adolphe Nshimirimana alikuwa rafiki wa karibu wa
rais Pierre Nkurunziza.
Hata baada ya kuondolewa kama afisa wa idara ya ujasusi
mwezi Novemba mwaka jana alikuwa akionekana na wengi kama
mwenye ushawishi mkubwa nchini humo.
Alishtumiwa kwa kusimamia oparesheni za kukabiliana na
waandamanaji baada ya rais Pierre Nkurunziza kutangaza kwamba atawania muhula
wa tatu mbali na kuhusika pakubwa katika kuzima jaribio la mapinduzi dhidi ya
rais huyo.
Kwa sasa wengi wana hofu ya hatua itakayochukuliwa na
wafuasi wa Nshimirimana.

