WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Makame Mbarawa amewahakikishia wananchi wa Pangani kwamba mwakani Serikali itaanza rasmi ujenzi wa barabara ya Lami kutoka Tanga, Pangani, Saadani hadi Bagamoyo yenye urefu wa kilomita 242 ili kuharakisha maendeleo wilayani humo.
Ahadi hiyo ameitoa wakati akijibu ombi la wananchi lililowasilishwa na Mbunge wa Jimbo la Pangani, Jumaa Awesso kwenye hafla ya uzinduzi wa Kivuko kipya cha MV Tanga pamoja na Gati la Pangani, miradi ambayo imetekelezwa kutokana na kodi za watanzania.
Amesema mradi wa barabara ambao unahitaji fedha nyingi utatekelezwa kwa awamu ambapo katika awamu ya kwanza ya ujenzi utahusisha kipande chenye urefu wa Km 47 kutoka jijini Tanga hadi mjini Pangani na kwamba fedha yake itatengwa katika bajeti ya mwaka ujao wa fedha wa 2017/2018 badala ya kusubiri kutafuta mkopo katika mpango uliowekwa hivi sasa.
Aidha mbarawa amesema ili kuwezesha mchakato huo wa awamu ya kwanza ya ujenzi wa barabara hiyo kufanyika kwa haraka wananchi wote ambao watalazimika kuhama ili kupisha mradi huo watalipwa fidia kwa mujibu wa sheria na si vinginevyo.
Awali Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Manase Le-kujan alisema ujenzi wa kivuko hicho uliofanywa na kampuni ya songoro marine umegharimu tsh. bln 4.02.
Kwa upande wake Kaimu Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), Karim Mataka akiwasilisha taarifa ya ujenzi wa Gati ya Pangani ambao umefanywa na Kampuni ya Alph Logistics Tanzania alisema umegharimu zaidi ya sh. Bilioni tatu na unatarajiwa kuboresha shughuli za uchukuzi kwa bandari ili kuwaunganisha wafanyabiashara wa miji ya Pangani, Pemba na Mkokotoni Zanzibar.