Jeshi la Polisi kanda Maalum Dsm limetangaza Operesheni kali dhidi ya wananchi walionunua Betri zinazoibwa katika minara ya Simu na kuwataka wananchi kuzisalimisha mara moja huku pia jeshi hilo likiwaonya wenye makampuni binafsi ya Ulinzi kuwafutia Vibali kutokana na baadhi ya askari wa kampuni hizo kushiriikiana na wahalifu na kufanikisha matukio mbali mbali ya wizi katika meneo mbali mbali jijini dsm.
Mkuu wa Operesheni wa jeshi la Polisi Kanda Maalum Dsm Lukas Mkondya Akizungumza na Viongozi na wawakilishi wa Makampuni ya Ulinzi jijini dsm amesema baadhi ya makampuni hayo yamekuwa wakiajiri askari wasiokuwa na sifa,wasio waadilifu na hawana mafunzo ambao wengi wao wamekuwa wakishirikiana na wahalifu kufanikisha matukio ya wizi kwa njia mbali mbali ikiwemo kupewa dawa za Usingizi.
Meneja Usalama wa minara ya Simu HTT – Abdalla Msika pamoja na Mkurugenzi wa Kampuni ya Ulinzi ya Kiwango wamesema hali ya wizi katika minara ya simu inatisha ambapo kwa wastani wa kila mwezi betri 100 huibiwa pamoja na Vifaa mbali mbali ikiwemo mafuta ya diseli ya kuendeshea minara hiyo.