Wananchi wa vijiji vinne kikiwemo cha Luzando Mkuranga wameukataa mpango wa upimaji wa ardhi kwa ajili ya mipango miji na kuiombaserikali kuingilia kati mgogoro kati ya mwekezaji anayedaiwa kumiliki zaidi ya ekari elfu mbili ambazo ndani ya eneo hilo kuna hati za watu zaidi ya watano na nyumba za makazi ya wananchi kwa zaidi ya miaka arobaini.
Wamepinga mpango huo baada ya kampuni ya ardhi Plan kuitisha mkutano wa wananchi ili kuwajulisha zoezi hilo saa chache baada ya mwenyekiti wa kijiji hicho kuwasomea barua iliyoeleza imetoka kwa mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mkuranga ikiwataka wananchi kuipa ushirikiano kampuni hiyo kupima ardhi zao kwa vile imepewa mamlaka kisheria.
Naye mwakilishi wa kampuni ya ardhi Plan alielezea namna walivyoelewana na mwekezaji hadi kufikia mchakato wa kutaka kupima ardhi hiyo na wananchi kuwakatalia.