Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji ipo katika hatua za mwisho za kuandaa mpango maalum wa kupima, kutambua na kuziwekea alama ya ubora bidhaa zinazoingia nchini lengo likiwa ni kuondokana na athari zitokanazo na matumizi ya bidhaa hizo, ikiwa hazikuthibitishwa.
Kaimu Mkurugenzi wa Uhamasishaji wa Biashara na Masoko kutoka Wizara hiyo Bw. Christopher Nassari amefahamisha mpango huo katika hafla ya kutoa leseni za Ubora kwa bidhaa 96 ambazo uzalishaji wake umekidhi matakwa ya viwango.
Amesema Mpango huo pia unalenga kuzitambua bidhaa za nje katika suala zima la ulipaji wa kodi ya mapato ya serikali na kudhibiti mianya ya uingizwaji holela wa bidhaa zisizokuwa na ubora katika masoko ya hapa nchini.
Ili kufanikisha mpango huo Shirika la Viwango Tanzania TBS limeanzisha kitengo maalum cha upimaji wa bidhaa hizo na kuziwekea alama maalum ya utambuzi, ambapo pia baadhi ya wazalishaji waliopata leseni za ubora wanatoa maoni.