WABUNGE wameahidi kuifanyia marekebisho sheria ya ndoa ya mwaka 1971 ambayo imekuwa kandamizi kwa watoto wa kike na kukiuka haki zao za msingi.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti mjini Dodoma jana katika semina ya wabunge iliyoandaliwa na Mtandao wa Kutokomeza Ndoa za Utotoni Tanzania (TECMN), baadhi ya wabunge walisema hatua hiyo itawakomboa watoto wa kike kuingia katika ndoa za utotoni kwani kuna madhara mengi yatokanayo na ndoa hizo ikiwamo kukosa haki ya kupata elimu.
Mbunge wa Chalinze (CCM ), Ridhiwani Kikwete, alisema wabunge na wazazi wapo tayari kuibadilisha sheria hiyo ili watoto wa kike wapate haki zao za msingi.
Alisema mabadiliko ya sheria hiyo yamechelewa na yeye kama mzazi ambaye ana mtoto wa kike anajiona ni mwathirika wa tatizo hilo katika siku za usoni.
“Lazima tubanane kubadilisha hii sheria kwa kuja na mapendekezo kutoka serikalini lakini siyo kwa utaratibu wa ‘White paper’ ambao Waziri Mwakyembe (Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Harrison Mwakyembe aliusema,” alisema.
Ridhiwani alisema ndoa za utotoni ni manyanyaso makubwa, hivyo wao kama wabunge wakilibeba suala hilo hakuna kitakachoshindikana.
Naye Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Dk. Mary Mwanjelwa, alisema wabunge wanaelewa ndoa hizo zinakiuka haki za watoto na zinawasababishia matatizo mbalimbali ikiwemo ya kiafya.
Alisema ndoa hizo zinaongeza vifo vya watoto na hata kina mama.
Kwa upande wake, Waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, alisema yeye kama waziri na mwanaharakati wa masuala ya haki za watoto anabeba jukumu la kufikisha maoni ya wabunge na mtandao wa TECMN serikalini.
Mwenyekiti wa mtandao huo, Valerian Msoka, aliwaomba wabunge na serikali kubadilisha sheria hiyo ili kusaidia kupunguza au kuondoa kabisa tatizo la ndoa za utotoni nchini.
Alisema pamoja na sababu nyingine zinazosababisha ndoa za utotoni, sheria nayo imekuwa moja ya kikwazo kinachokwamisha kutokemeza tatizo hilo.
Alisema kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Kuhudumia Watoto Duniani (Unicef) za mwaka 2012), mikoa inayoongoza kwa ndoa za utotoni nchini ni Shinyanga ukiongoza kwa asilimia 59, ukifuatiwa na Tabora asilimia 58, Mara asilimia 55, Dodoma asilimia 51 na Lindi asilimia 48.
Mingine ni Mbeya asilimia 45, Morogoro asilimia 42, Singida asilimia 42, Rukwa asilimia 40, Ruvuma asilimia 39, Mwanza asilimia 37, Kagera asilimia 36, Mtwara asilimia 35, Manyara asilimia 34, Pwani asilimia 33, Tanga asilimia 29, Arusha asilimia 27, Kilimanjaro asilimia 27, Kigoma asilimia 26, Dar es Salaam asilimia 19 na Iringa asilimia 8.