Bomoa Bomoa: Wakazi wa Kariakoo Dar, walivyopewa saa mbili kuondoka


Zoezi la bomoa bomoa la waliojenga ndani ya mita 30 kupisha ujenzi wa reli ya kisasa leo limehamia eneo la Kariakoo Gerezani jijini Dar es salaam, ambapo majengo kadhaa yamevunjwa,ikiwemo kituo cha mafuta lakini pia wafanyabiashara wa soko la Kibasila wamepewa masaa mawili kuondoka.

Katika eneo hilo la soko la Kariakoo wafanyabiashara hao walionekana kuchanganyikiwa kutokana na taarifa ya kuwataka kuondoka katika kipindi cha saa mbili ikizingatiwa wengi wao walikuwa wamepumzika majumbani mwao.

Channel ten ilifika eneo hilo na kushuhudia harakati za wafanyabiashara hao kuhamisha mali zao huku wakilalamikia kutokuwa na taarifa lakini pia wasijue sehemu za kupeleka mali zao.

Kiongozi wa soko hilo Hassan Namkwacha amesema awali walipata taarifa ya kubomolewa ndani ya mita 30 ambapo walikubaliana na agizo hilo lakini wameshangaa kutakiwa kuondoka eneo hilo katika kipindi cha masaa mawili na kudai kuwa eneo hilo wamekuwa wakifanya shughuli zao na kulipa kodi za mamlaka za jiji .
Mpya zaidi Nzee zaidi