Maafisa katika idara ya masuala ya dharura wafahamisha vifo vya watu 20 baada ya mti mkubwa kuanguka eneo moja la maporomoko ya maji nchini Ghana .
Mti huo umeripotiwa kuanguka baada ya upepo mkali kuzuka na kuangukia wanafunzi kutoka shule ya upili ya Wenchi waliokuwa wanaogelea katika maporomoko ya maji ya Kintampo.
Prince Billy Anaglate afisa mkuu wa idara ya huduma ya ajali za moto aliambia shirika la habari la AFP kuwa 18 ya wanafunzi walifariki papo hapo huku baadaye wengine wawili wakafariki hospitalini.
Alifahamisha kuwa watu wengine 11 waliojeruhiwa wanaendelea kupata matibabu miongozni mwao ni kiongozi wa wanafunzi hao walioandaa ziara hiyo ya wanafunzi.
Waziri wa utalii wa Ghana Catherine Abelema Afeku alituma salamu za rambi rambi kwa familia za wanafunzi waliofariki na kuombea waliojeruhiwa kupona haraka .
Maporomoko ya maji ya Kintampo ni eneo maarufu la kitalii linalopatikana kanda ya kati ya Ghana .