Saikolojia ya Roma
Mkatoliki na wenzake bado ipo kwenye hali ya
kuteswa na kutekwa alikotendewa hivi karibuni na watu wenye nia ovu.
Namkumbusha Roma
Mkatoliki na wenzake Bin Laden pamoja Monii kuwa hata Yesu Kristo siku kama ya leo alikuwa amepatiwa mateso makali kutoka kwa
wayahudi wenye maono ya kiudharimu na wasiopendezwa na haki.
yesu alitendewa hayo yote kutokana ukumbozi kwa watu wengine ili kusimama kwenye kuamini ujumbe wake.
yesu alitendewa hayo yote kutokana ukumbozi kwa watu wengine ili kusimama kwenye kuamini ujumbe wake.
Roma ni Msanii mwenye kupaza sauti za wanyonge na
kuzungumzia sana masuala yanayohusu maslahi ya
umma hivyo kama ulitekwa kwa sababu hizo upo
kwenye njia ya yesu.
Nakumbuka vibao vyako na
mashairi yako kadhaa ambayo uliimba kwa uchungu na uzalendo bila kutafuna
maneno uliimba kuhusu mustakabari masuala kadhaa.
Hukuacha kupaza suati
kukemea ufisadi tangu uliponza kazi hii ya sanaa kupitia muziki wa Hip Hop.
Roma itoshe tu kujikubali
kuwa wewe ni Mwanakondoo uliyepitia mtihani huu na kwamba wanaobeza kitendo
ulichofanyiwa wewe yatwakuta tumerithi misemo kutoka ka malenga wetu isemayo ukimuona mwenzako ananyolewa nawe tia
maji kchwa chako,