Na. Ahmad Mmow,
Lindi. KUELEKEA nchi ya viwanda na uchumi wa kati. Shirika la wanga wa mihogo Tanzania (cassava starch of Tanzania) linatarajia kuanza kujenga kiwanda cha kusindika mihogo kuanzia mwezi Oktoba mwaka huu.
Hayo yamebainishwa leo na mkuu wa idara ya rasilimali watu na ushirikiano wa shirika hilo, Knowles Lumambo alipozungumza na blogi hii ofisini kwake katika manispaa ya Lindi. Lumambo ambae pamoja na kutoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali kuhusu uwekezaji utakaofanywa na shirika hilo, alisema ujenzi wa kiwanda hicho kitakachotengeneza unga wa mihogo na wanga kitaanza kujengwa mwezi Oktoba mwaka huu na kukamilika mwakani.
Nakulitaja eneo litakalo jengwa kiwanda hicho kuwa ni katika kijiji cha Mbalala tarafa ya Mtama wilaya ya Lindi. "Hivi sasa tunasubiri invoisi(hati ya madai) ya gharama na fidia kwa ajili ya hekta arobaini zitakazo tumika kwa ujenzi wa kiwanda hicho," alisema Lumambo. Alisema vifaa kwa ajili ya ujenzi huo vitawasili wakati wowote kuanzia sasa. Huku akibainisha kuwa wanaamini zoezi la kupata ardhi kwa ajili ya kilimo cha zao hilo na ujenzi wa kiwanda hicho litafanikiwa..
Akizungumzia suala la malipo ya fidia kwa wananchi waliokubali kutoa maeneo yao ya ardhi kwa ajili ya mradi huo, Lumambo alisema :Tunaendelea kulipa, kwasasa wananchi wa kijiji cha Linoha wanaweza kuanza Kulipwa, kwani kimsingi taratibu za malipo yao kwa upande wetu zimekamilika, tukiwalipa hao tutakuwa tumebakiwa na vijiji viwili tu. Kwani tayari tumeshalipa katika vijiji vya Lipome, Lindwandwali na Nahukahuka B, tayari. Bado Nahukahuka A na Mandwanga, 'alibainisha Lumambo.
Mkuu huyo wa idara alisema miongoni mwa sababu zilizosababisha kuchelewa malipo hayo ni mabadiliko ya uongozi kwenye vijiji ambavyo wananchi wake walikubali kutoa ardhi kwa ajili ya kupisha mradi huo. Nakuongeza kusema halmashauri ya wilaya ya Lindi imeridhia kutoa hekta 6050 zitakazo tumika kwa ajili ya kilimo cha mihogo.
Ambapo sasa shirika hilo limepata hekta 3004.011 katika vijiji vya Linoha (456.507),Lipome (502.420),Nahukahuka A(634.614),Nahukahuka B(411.795), Lindwandwali (461.773) na Mandwanga hekta 536. 902.Alitaja faida za mradi huo kuwa ni kuongeza thamani ya zao la mihogo ambalo hivi sasa linaonekana halina thamani katika kuongeza mapato ya nchi kupitia kodi, kutoa ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja kwa wananchi na kutekeleza mpango wa serikali wa kuifanya nchi kuwa ya viwanda.
"Mradi huu tulitarajia ungeanza tangu mwaka 2014, hata hivyo mchakato wa kupata ardhi ni mrefu, hatahivyo tunataraji kila kitu kitakwenda sawa. Ndio sababu tumeanza kuweka vitalu vya mbegu. Huku tukianza maandalizi ya ujenzi wa kiwanda hicho ambacho kitatengeneza unga na wanga, "alisisitiza Lumambo. Mkoa w Lindi ni miongoni mwa mikoa michache yenye ardhi ya kutosha kwa shuguli za kilimo. Ambapo kwa sasa mazao makuu ya biashara yanayozalishwa kwa wingi katika katika mkoa huu ni korosho na ufuta.